Description

Kozi hii ni ya kwanza kati ya mbili katika masomo yako ya barua za Paulo kwa Wagalatia na Warumi. Unaanza na Wagalatia kwa sababu inaweka msingi wa kusoma kwako Warumi.

Katika kozi hii utajifunza barua ya Paulo kwa Wagalatia. Utaangalia hali ya kihistoria na utazingatia maswala muhimu ya kitheolojia katika kanisa la kwanza ambalo Paulo alishughulika. Utafahamu vyema maisha, tabia, na huduma ya mtume Paulo. Pia utapata ufahamu mpya katika maisha ya Kikristo na huduma unavyotumia mafundisho ya waraka huu kwa hali za kisasa.